Saturday 16 July 2016

UNAPATA HEDHI ZENYE MAUMIVU? SULUHISHO LIPO HAPA(PAINFUL MENSTRUATION- DYSMENORRHEA)

HEDHI SALAMA ZISIZO NA MAUMIVU

Helleminigilder Ndangalasi (MD student Muhimbili university of health and allied sciences)
0030hrs 16th July 2016

Labda sio mara nyingi lakini nimekutana na wanawake mbalimbali wakilalamika kuhusu kupata hedhi zinazoambatana na maumivu kile watalamu wanaita “dysmenorrhea”. Mimi mwenyewe nikiwa mhanga wa hili mara nyingi mpaka pale nilipopata suluhisho. Ndipo nilipojua, anha… Kumbe na mimi naweza kupata hedhi zisizokuwa na maumivu yoyote.
BASI LEO TUTAJIBU MASWALI MAKUU MAWILI:
1.NINI KINASABABISHA MAUMIVU HAYA?
2. NTAFANYAJE KUPATA SULUHISHO LA HII HALI?

Karibu tuzungumze,

Hedhi kwa kawaida , ile damu hutoka kwasababu yai ulilotengeneza ili lirutubishwe na shahawa za mwanaume kwa bahati mbaya halijarutubishwa hivyo hilo yai pamoja na kuta za mfuko wa uzazi zilizoandaliwa kumpokea mtoto ambaye angeanza kutengenezwa vinatolewa sababu havina kazi tena kwa mda huo. Labda kwasababu haukujamiiana na mwanaume yai lilipotengenezwa au labda mlitumia kinga hivyo shahawa hazikufika kwenye yai.

 Maumivu kwenye hedhi husababishwa na kemikali mwilini kitalamu zinaitwa “prostaglandins”. Hizi kazi yake kubwa ni kufanya misuli ya mfuko wa uzazi (uterus) kukakamaa kana kwamba kuna mtoto mwanamke ajifungue. Ndizo hata zinaleta uchungu wa mama anayetaka kujifungua. Sasa kwa baadhi ya wanawake wakati wa hedhi, kemikali hizi hutengenezwa hivyo kufanya misuli hii ya mfuko wa uzazi kukamaa kuliko kawaida mpaka kupelekea maumivu.

TUFANYEJE KAMA WANAWAKE?

Kabla sijasema hili kwanza naomba tukumbushie tu haraka haraka jinsi ya kuhesabu mzunguko wa hedhi ambao kwa kawaida ni wa siku kama 28 hivi.
Je, unakumbuka mara ya mwisho ulivyopata hedhi? Hi indo ilikua siku ya kwanza ya mzunguko huo. Hedhi huwa zinaweza kuchukua siku 3 mpaka 5 kwa wengine. Siku ya 14 kuanzia siku ya kwanza ya hedhi au siku moja kabla au baada ndipo yai linatolewa tayari kurutubishwa. Kama likirutubishwa, utapata ujauzito lakini kama lisipo rutubishwa tunategema litatoka kama hedhi baada ya siku kama 14 nyingine utakapoanza mzunguko mpya. Jumla huwa siku kwa kawaida 28 ingawa zinaweza kuongezeka au kupungua kutokana na vitu kama msongo wa mawazo(stress) lakini ni vizuri ukamwona daktari kwa uchunguzi zaidi.

Ukiwa unapata hedhi zenye maumivu KAMWE USIKIMBILIE KUNYWA DAWA ZA KUTULIZA MAUMIVU KAMA PANADOL HASA BILA USHAURI WA DAKTARI, TUMIA PALE UNAPOSHAURIWA NA DAKTARI TU.
   
Jiwekee utaratibu wa kufanya mazoezi ya mwili siku zinazokaribia siku ya 14, kuanzia siku ya 12 mpaka 16 hivi. Ruka Kamba , kimbia ukiweza n.k. Vizuri kama ukifanya mazoezi kuwa sehemu yako ya maisha kabisa ukiachana na siku za hedhi tu, ina umuhimu mkubwa wa kiafya pia ukizingatia itakutengezea mwili unaovutia.
TUFANYE MAZOEZI. MIMI NACHEZA BASKETBALL, WEWE JE? #MSOLWA SEC SCHOOL
Vaziri et al.,(2015) anatuambia, ”Both aerobic and stretching exercises were effective in reducing the severity of dysmenorrhea. Therefore, women could choose one of these two methods with regard to their interest and lifestyle.”

Mtalamu mwingine aliyafanya tafiti yake kwa kuangalia mazoezi ya Yoga yanapunguzaje hedhi zenye maumivu akahitimisha kuwa,” yoga interventions may reduce menstrual cramps and menstrual distress in female undergraduate students with primary dysmenorrhea”.(Yang & Kim, 2016)

Pia Ortiz et al (2015) anasema ,”Strengthening, stretching and muscle relaxation techniques, in addition to jogging, are effective for reducing dysmenorrheic symptoms when they are regularly performed.”

TAHADHARI: MAUMIVU YAKIZIDI AU YAKIENDELEA MUONE DAKTARI HARAKA, KUNA UWEZEKANO WA MAGONJWA MENGINE KUWA CHANZO KAMA “ENDOMETRIOSIS” (TUTAZUNGUMZIA SIKU NYINGINE)

Tafadhali wasiliana nasi, tujulishe kama imekusaidia na pia kama una maswali.
 Mpaka tutakapokutana siku nyingine.

Asanteni sana

References:
Ortiz MI1, Cortés-Márquez SK2, Romero-Quezada LC3, Murguía-Cánovas G4, J.-D. A. (2015). Effect of a physiotherapy program in women with primary dysmenorrhea. Retrieved from http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/26319652
Vaziri, F., Hoseini, A., Kamali, F., Abdali, K., Hadianfard, M., & Sayadi, M. (2015). Comparing the effects of aerobic and stretching exercises on the intensity of primary dysmenorrhea in the students of universities of bushehr. Journal of Family & Reproductive Health, 9(1), 23–8. Retrieved from http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/25904964
Yang, N.-Y., & Kim, S.-D. (2016). Effects of a Yoga Program on Menstrual Cramps and Menstrual Distress in Undergraduate Students with Primary Dysmenorrhea: A Single-Blind, Randomized Controlled Trial. Journal of Alternative and Complementary Medicine (New York, N.Y.). http://doi.org/10.1089/acm.2016.0058


No comments:

Post a Comment