Sunday 28 August 2016

Electronics(part 3-Telecommunication)-lesson 7

This is part 3 and last part in the topic of electronics in this Ntanguligwa Online advanced series! Telecommunication is extensively covered. Its a very interesting topic.

 Welcome. Contact:0714949061(whats app), 0785071020

Wednesday 24 August 2016

ADHABU NA MABADILIKO YA TABIA-AFYA

ADHABU AU MAONYO KATIKA KUBADILI TABIA YA MTU
Constantine Ntanguligwa(MD student Muhimbili university of health and allied sciences)
 1215hrs 24th August 2016

Karibu tuzungumze:

Ni wangapi tumechapwa na wazazi wetu baada ya kukosea nyumbani? Ni wangapi tumepigwa na rula vidoleni na mwalimu mwalimu wa hesabu pale ambapo tumekosea kujumlisha darasani? Ni wangapi tumewanyima chakula wafanyakazi wetu wa ndani sababu alisahau kumbadilisha mwanao nepi? Lakini pia, ni wangapi wamewachoma moto vidole watoto wao kwasababu ya udokozi?

Labda kabla sijaanza, niseme kwanini nimeamua kuongelea kuhusu adhabu leo. Afya ya binadamu, Si pale tu ambapo mtu anaumwa au kutokuumwa magonjwa mbalimbali kama malaria. Afya hujumisha maisha yote ya mwanadamu. Hali yake kimwili, kiakili(kisaikolojia), mazingira anayoishi na jamii kwa ujumla. Vyote hivi ni "afya" ya mwanadamu.

Adhabu ni kitu kinachotambulika na kukubalika katika ulimwengu wa wanasaikolojia. Adhabu hutumika kama njia ya kufanya mtu asirudie kosa endapo tu itatolewa kwa usahihi. Leo tutajua nakujibu maswali yafuatayo:

  1. ADHABU INAWEZA KUSABABISHA KOSA LISIRUDIWE AU KUTOSABABISHA MABADILIKO YOYOTE, JE ADHABU INATAKIWA KUWA VIPI?
  2. BAADA YA KUTOA ADHABU, JE KUNA KITU NATAKIWA KUFANYA ILI NIHAKIKISHE INAFANYA KAZI INAVYOTAKIWA?
Kwa mazoea, huwa tunamfanyia mtu vitendo au matukio yasiyomridhisha au yasiyompendeza au yanayokatisha tamaa mtu mara tu baada ya kufanya kosa au kuonesha tabia mbaya ambayo hupelekea mabadiliko ya tabia hiyo. Huweza kuwa faini, kufungwa, kupigwa, kufelishwa, kufukuzwa kazi/shule na kupewa barua ya onyo. Vitu hivi huitwa "aversive events" kwenye saikolojia, hili ni somo lefu linalojitegemea.

Adhabu ni kitendo yakuikandamiza tabia mbaya kwa kufanya vitendo hai(active supression). Adhabu si lazima ilete maumivu kwa mtu. Adhabu hutofautiana kuanzia zile zinazoleta madhara madogo mpaka zile zinazoweza kupelekea ulemavu wa mtu kabisa ila mwisho wa siku lengo la mtoaji likiwa kubadili mienendo mibaya kwa mlengwa.

Adhabu huweza kuwa kwa mifumo mitatu au aina tatu:
  • "Aversive events" kama nilivyoielezea hapo juu.
  • Kuondoa faida zinazodhaniwa kuwepo na muhusika au raha baada ya kufanya kosa flani au kuwa na tabia mbaya. Hasa kwa watoto.
  • Kufanya kazi ili kukandamiza tabia flani.
1.AVERSIVE EVENTS:
Hizi hugawanyika sehemu mbili. 
  • Sehemu ya kwanza ni pale ambapo utamfanyia mtu kwa vitendo atakavyohisi kwa kuona au kugusa(physical perception) mfano kwa mupata maumivu. Kama vile kumchapa fimbo au kumfinya masikio kama ni mtoto.
  • Sehemu ya pili ni pale ambapo utamfanyia vitu atakavyohisi kiakili kuwa si sahihi mfano, pale atakapotaka kufanya kosa halafu ukatikisa kichwa kumaanisha hapana. Pale atakapofanya kosa halafu ukakunja uso akajua umekasirishwa na anachofanya hivyo hutambua akilini mwake na kuacha mara moja, pale atakapofanya kosa halafu ukamnyoshea kidole au pale atakapo kuomba kwenda club na ukamwambia hapana kila mara mwisho wa siku ataona kuwa hauridhishwi nacho kisha akaacha kukuomba.
2.KUONDOA "FAIDA"/RAHA
Kama nilivyosema hapo awali kuwa, kuna watu ambao hufanya makosa au huwa na tabia mbaya inayoendelea kwasababu kuna faida anayoiona yeye anaipata baada ya kufanya hayo. Mfano mtoto asipofanya kazi za shuleni nyumbani kwasababu ya TV ukamkataza kuangalia TV kwa wiki moja. Atahisi anapitwa kama ni tamthilia na mara nyingine hatarudia hasa atakapofika shuleni na kukuta wenzake wanasimuliana kilichotokea kwenye tamthilia jana yake. Kama anapewa Ada akalipe na halipi kwa wakati na kwenda kufanya matumizi yake na hatimaye kukopa kwa wenzake na kulipa ada kwa kuchelewa labda kwa mazoea kuwa hafanywi kitu akimwelezea("kumdanganya danganya kwa maneno kidogo") mwalimu mkuu huwa anamuacha hivyo mnaweka faini kubwa isiyohitaji maelezo ambapo ataacha kwa kuona hamna maelezo tena yanayosikilizwa bali ni faini tu. Au kutoruhusiwa kuja shule mpaka utakapolipa hata kama unasababu ya msingi ya kutolipa.

3.KUFANYA KAZI
Hapa ni pale mtu anapofanya kosa au kuonesha tabia mbaya na kufanyishwa kazi kama malipizi ya tabia hiyo. Kazi hii mara nyingi huhusiana moja kwa moja na kosa lile na huweza kuwa kulazimishwa kufanya kinyume chake. mfano, mtu anapotupa takataka ovyo nje, utamwambia asafishe uwanja wote. mtoto anapomwaga chakula mezani makusudi huweza kuambiwa asafishe meza na kudeki sehemu wanayotumia kula, lakini pia mtu anapokosea kuandika jina lake utamwambia aliandike kwa usahihi mara 50.

Kunakitu tunaita "reinforcements"/viimarishi. Zenyewe hutumika kuendeleza tabia fulani. Mfano, mtoto wako anapofaulu halafu ukampa zawadi ya kitu alichokuwa anakitamani sana, hii itamjengea hamu ya kuendelea kufanya juhudi za kufaulu aendelee kupata zawadi hizo. Si lazima kutoa vitu, unaweza kuimarisha tabia kwa kunyima pia. Mfano, kama wafanyakazi wako wana sheria ya kumaliza kazi ijumaa na kwa wasiomaliza kwa wakati hutakiwa kurudi kazini wikendi lakini wanaomaliza ijumaa wanapata likizo wikendi. Kuwambia warudi wikendi ni kuwanyima uhuru ambao utapelekea kufanya kazi kwa bidii na kuimarisha tabia hii ya kumaliza kwa wakati.

TOFAUTI YA REINFORCEMENTS/VIIMARISHI NA PUNISHMENT/ADHABU: viimarishi hulenga hasa kuimarisha tabia fulani na adhabu hulenga kukandamiza tabia flani.

Hivi vinaingiliana na huweza kuchanganywa lakini ni vitu tofauti. Hii inamaanisha ni vema vitu hivi viwili vikatumika kwa pamoja. Mfano, mtoto anapokuwa na kiburi, unaweza kumchapa fimbo na matokeo yake anaweza kukuchukia na kukuona mbaya lakini kwa yale mazuri aliyonayo ukimpongeza baadaye atabadilika na kukuona kumbe si kama alivyokudhania una malengo mazuri na yeye. Hivyo inashauriwa kutumia njia zote mbili. Hivyo ni vema baada ya adhabu ukatafuta njii ya kuimarisha tabia nzuri uliyolenga kuijenga.

MADHARA YA ADHABU:
Madhara ni mengi kutokana na njia unayotumia hasa ikiwa si sahihi. mfano kuchukiwa, kukimbia shule, kutoroka nyumbani, kulia sana, kisasi na nidhamu ya woga.
Mfano, mtoto wako ni mwizi na mdokozi:
 Mtu mmoja yeye amemchoma moto vidole na mwingine amemchapa fimbo.
  •  Aliyemchoma vidole kuna hatari kubwa mwanao akakimbia nyumbani na pengine kwenda kuendeleza wizi huko anapoenda.
  •  Lakini, anayemchapa anafanya njia sahihi kwani ni uzito unaostahili kwa kesi hii na ni vema zaidi baada ya hapo ukaangalia chanzo cha kwanini mwanao ni mdokozi.                                  
Pengine wewe mzazi humuweka kwenye vishawishi vya kumuacha mwanao aende shule wenzake wakiwa wanakula wewe humpi hela ya matumizi shuleni na kuishia kuwaibia wenzake huko shuleni au hata kuiba nyumbani anapoona hela. Lakini utakapokuwa unamfungashia mfano chakula anachokipenda shuleni na kumpa hela ndogo ya matumizi kama atanunua pipi mfano utakuwa umetoa adhabu na umeimarisha(reinforce) tabia nzuri unayotaka awe nayo.

Mfano mwingine, mwanao hasomi na kagoma kwenda shule kwasababu anaamini kuwa wapo wengi wamefanikiwa na hawajasoma nakukukupa mifano kama Diamond Platnumz, Ronaldo na Messi. 

  • Mmoja akamwambia mwanae kama hutaki kusoma ondoka kwangu nisikuone ambayo ni adhabu tayari kumfukuza kwako hapa.
  • mwingine akamwambia mwanaye kuwa usinipande kichwani, kwa kuwa wewe ni mwanangu utafanya yale ninayokuongoza mimi na utakapofika umri wa kujitegemea fanya utakacho amua lakini si kwa sasa hivyo unaenda shule na nakupa kazi ya kuniandikia watu kumi waliofanikiwa bila kusoma na kumi waliofanikiwa kwa kusoma, uorodheshe historia za maisha yao na mwisho uainishe wapi waliofanikiwa kirahisi na kupita njia rahisi kufikia mafanikio yako. 

Tunakubaliana kuwa wote wanaweza kuwa sahihi kulingana na mazingira ingawa wa kwanza anaweza kumpa ushawishi mwanae kutoroka nyumbani na hata hivyo maisha yakimshinda huko atarudi amejifunza lakini huyu wa pili ametoa suluhisho lenye kiimarishi/reinforcements kwani kwa kuandika hayo aliyomwambia atajifunza kuwa shule ni chaguo zuri zaidi lenye unafuu zaidi.

HIVYO UNAPOTOA ADHABU NI VEMA UKATAFUTA NAMNA/UPENYO WA KUTOA KIIMARISHI TABIA PIA(REINFORCEMENT)

VIBOKO SHULENI:
Serikali imeagiza viboko kutotumika shuleni. Wakitoa sababu kuwa inasababisha utoro shuleni. Hii ni kweli kabisa kulingana na namna viboko hivyo vilivyokuwa vinatumika kwa baadhi ya walimu kusaka heshima ya lazima au sifa bila kuzingatia matumizi sahihi ya viboko hivyo.
Viboko vikitumika shuleni, huweza kuwa na msaada mkubwa kwa wakati sahihi, kwa kiasi sahihi na kwa nia ya dhati.

Cha muhimu, tutumie adhabu sahihi lengo likiwa kubadilisha tabia za watu na kuzuia madhara yaliyosababishwa kutokea tena. Chanzo kiangaliwe na reinforcement(viimarishi tabia) vihusike kwenye vyanzo hivyo.

Swali: Wazazi wanaotumia adhabu zilizozidi kipimo, watoto wao huwa watukutu zaidi. Je hii ni kweli?
Until next time.





Tuesday 23 August 2016

Electronics(part 2)-lesson 6

Welcome and feel at home:In this lesson 6. Ntanguligwa online brings to you Electronics part 2 out of 3 which thorough covers:Transistors and OPAMPS



Feel free anytime to contact me 0785071020 normal text and 0714949061 whats app!



Welcome. Thank you.



Thursday 18 August 2016

VICIOUS CIRCLE OF SOCIAL DETERMINANTS OF HEALTH

HEALTH AND THE CURATIVE APPROACH
Constantine Ntanguligwa(MD student Muhimbili university of health and allied sciences)
 0945hrs 18th August 2016

Karibu tuzungumze:

Kwanza nianze kwa kuelezea maana ya "vicious circle". Huu ni mzunguko wa mfumo kama wa duara unahusisha kitu flani na sababu zake kuwa na mwendelezo usioisha. Tunaposema "vicious circle of social determinants of health" tunamaanisha duara linaloanza na Afya yako na yale yote yanayoweza kufanya afya yako kuwa bora au kuidhoofisha katika uhusiano usio na kikomo. Ni dhahiri kwamba, duara huzunguka bila mwisho

Pili, tunaposema "curative approach" huu ni mfumo wa ki-tiba ambao hukazia zaidi kwenye matibabu ya mgonjwa mwenyewe moja kwa moja, mfumo ukizingatia hasa vijidudu vinavyokufanya uumwe na vyanzo. The center of focus kwenye mfumo huu wa tiba vina concentrate zaidi kwa vimelea kama chanzo kikuu cha magonjwa (parasites and vectors as primary to health). Huu ndo mfumo tunaotumia katika sekta yetu ya afya hapa.



Watalamu wa sayansi ya tabia(behavioural sciences) wanatuambia, vitu vilivyo msingi kwa afya ambavyo ndivyo vitakavyoamua afya yako kesho itakuwaje(social determinants of health), si mbu wala nzi wala vimelea vya homa, lakini ni hivi vifuatavyo:

1.LIFE STYLES(mienendo ya maisha yetu)
Hizi ni tabia/mienendo yetu ya kila siku. Je, tunakunywa pombe sana? Je, tuna wapenzi wengi? Je tunafanya ngono zembe? Je,tunakula kabla ya kunawa? Hii yote ndiyo itakayoamua afya yako wewe itakuwaje, kama ni magonjwa ya zinaa yatakuwa rafiki yako au homa ya tumbo na kipindupindu. Sigara inauwa watu milioni 6 kila mwaka inazidi idadi ya watu wanaokufa kwa UKIMWI, TB na MALARIA ukijumuisha kwa mwaka.
JE, MIENENDO YETU YA MAISHA NI RAFIKI KWA AFYA ZETU?



2.AGE(umri)
Umri unachangia sana baadhi ya magonjwa. Mfano, si ajabu kuanzia umri wa miaka 30 na kuendelea kupata magonjwa ya moyo, figo, kisukari na presha, labda kwasababu ya misuli na mishipa ya damu kuanza kuchoka. Si, ajabu watoto wadogo kupata minyoo labda kwasababu ya kula kila wanachoweka mikononi bila kujua hali ya usafi na usalama. Si ajabu vijana wengi kuwa wahanga wa magonjwa ya zinaa na madawa ya kulevya labda kutokana na ushawishi wa makundi na tamaa. Si ajabu vijana wengi kuwa wahanga wa ajali za boda boda labda kwasababu wao ndo watafutaji maisha wakubwa katika umri huo.
JE, TUNATAMBUA UMRI WETU HUWEZA KUPATWA NA MAGONJWA GANI ZAIDI NA YALE YA WATOTO WADOGO WANAOHITAJI USIMAMIZI WETU?


3.CULTURE(tamaduni)
Hapa ndipo zinapokuja mila na desturi. Hivi ni kweli unakubali kurithishwa mke wa kaka yako bila kujali uhusiano wao ulikuwaje? kama ana ukimwi je? Ni kweli mila na desturi zetu zinatuambia tukae na wanyama wetu ndani ya nyumba zetu? Usalama wa magonjwa ya wanyama kutokua yetu uko wapi?
Ni kweli watoto wetu wa kike wanakeketwa mpaka leo hii? Afya yao ya uzazi, saikolojia na magonjwa ambukizi i hali gani? Hivi ni kweli kuna makabila ambayo kumpiga mke wako ni lazima, kufanya uzazi wa mpango ni mwiko na kujifungulia nyumbani ndo mpango mzima? Nani kama mama inakujaje sasa hapo? Pamoja na mila na desturi nyingine nyingi sana.
JE, UKO TAYARI KUBADILI MILA NA DESTURI ZINAZOHATARISHA AFYA YAKO NA MAISHA SASA?


4.GENDER(jinsia)
Ni kweli kabisa, ukiwa mwanaume kuna magonjwa yanayokuhusu na ukiwa mwanamke kuna ya kwako pia. Hivyo, kuwa na jinsia tayari na chanzo cha magojwa fulani mfano kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi kwa wanawake lakini pia tatizo la nguvu za kiume kwa wanaume. Labda ndo maana tunawatalamu kama wanaoitwa madaktari wa kina mama(gynaecologists). Takwimu zinaonesha pia kuwa, wanawake hutembelea hospitali mara nyingi zaidi kuliko wanaume. Labda kwasababu wanamatatizo mengi zaidi au kwasababu wanaume hujikuta wako imara na kwenda hospitali utaonekana dhaifu. Labda nikwambie tu kuwa, kirusi cha ukimwi kikikuingia, hakijali wewe ni mwanaume au mwanamke.
JE, TUNATAMBUA MAGONJWA YANAYOIKUMBA JINSIA YETU(ANGALAU MACHACHE MUHIMU) ILI KUJILINDA?

5.EDUCATION(elimu)
Ni kweli, mtu ambaye ameenda shule walau elimu ya msingi ni tofauti sana na yule ambaye hajaenda kabisa. Angalau nikiwaangalia wadogo zangu mmoja yupo chekechea na mwingine darasa la nne, kabla ya kula wana nawa mikono. Wanajua maji wanayotakiwa kunywa inabidi yachemshwe kwanza. Wewe mwenye elimu kubwa zaidi tunategemea uwe na uelewa mkubwa zaidi na uwezo wa kuepuka vyanzo vya magonjwa vinavyoepukika. Maajabu yanakuja pale ambapo leo hii mwanafunzi wa form 6 anapokunywa maji ya bomba bila kuchemsha au mwanafunzi wa chuo kikuu anapokula bila kunawa. Hadi hili tutailaumu serikali kuwa kuna mfumo mbovu wa elimu? Ni uzembe na kutozingatia yale tunayoyajua. Namna hii magonjwa yataendelea kuwa rafiki zetu. Leo hii nchi kama Denmark ukiona mbu basi ni utalii umefanya. Malaria ni historia. Kwanini uwe ghala la vimelea na elimu yote uliyonayo? Basi fanya vile vinavyowezekana kutokana na elimu uliyopata uepuke baadhi ya magonjwa. Elimu si ya darasani tu, familia ndiyo shule ya kwanza kwenye maisha ya binadamu. Kuwa msimamizi wa afya nyumbani na mahali unapoishi.

JE, ELIMU ULIYONAYO INAKUSAIDIA KUWA NA AFYA YA TOFAUTI NA ASIYEKUWA NAYO?


6.WORKING CONDITIONS(mazingira ya kazi)
Ni kweli wanasema, mfanikiwa hachagui wala kubagua kazi. Ni kweli hali za maisha yetu zinaweza kutupelekea kufanya kazi zinazoweka afya zetu matatani, na mara nyingine ipo nje ya uwezo wetu. Mtu unapolazimika kufanya kazi kama msafisha jiji, mda wote uko na uchafu wa jalalani, unafanya kazi kiwanda cha cement au mashine ya kukoboa mda wote uko na vumbi kali au kwenye minara ya simu mda wote upo kwenye mionzi hatarishi kwa kansa. Muhimu ni kuzingatia utendaji wa kazi tujilinde inavyowezekana. Kama ni jalalani, tuvae gloves, kama ni mionzi tujitahidi kupunguza kukaa maeneo hayo bila sababu, kama ni vumbi kali tukumbuke kuvaa mask usoni. Mwingine atasema, kama ni kahaba au changudoa uvae kondomu ujilinde. Inaweza kuwa sawa unajilinda lakini hiyo ni tofauti. Kama ni kazi fanya kazi halali zenye risk kidogo sababu hatari ipo katika kazi zote zinatofautiana tu uzito. Hata daktari yupo kwenye hatari kubwa ya maambukizi kutoka kwa wagonjwa.
JE, UNAFAHAMU MAZINGIRA YA KAZI YAKO YANA HATARI GANI KWA AFYA YAKO?
 


7.NUTRITION(vyakula):
Mwili wetu hufanya kazi vizuri pale tu ambapo tutakuwa tumeshiba vizuri. Ni wangapi wanaweza kukaa kwa makusudi siku nzima masaa 24 bila kula chochote wakaishi bila shida yoyote, comfortably. Mara zote tutahitaji kula, je tunakula nini? Mlo wetu unafaa kuitwa chakula bora. Tunatakiwa kula matunda kwa sana, kunywa maji kwa sana na kuhakikisha mlo wetu una mahitaji yote katika kiasi sahihi. Wanga kidogo(vyakula kama mihogo,ugali,wali na viazi), protini kigodo(samaki,nyama,mayai), mafuta kidogo(karanga,vyakula vya kukaanga kama chipsi), vitamini(mboga za majani na matunda). Tujitahidi tuwe tunapata hivi angalau kila siku na kupunguza ulaji wa vyakula vya mafuta na kuongeza matunda(somo hili refu kidogo tutalitafutia makala yake).

JE, WANGAPI SISI MLO NI CHIPSI,KUKU,PIZZA NA BURGER TU MASAA 24 SIKU SABA KATIKA WIKI. TUNAJIANDAA KUWA DILI KWA MADAKTARI WA MOYO?

8.ENVIRONMENT(mazingira)
Uchafuzi wa mazingira ni tatizo kubwa sana katika nchi zetu zinazoendelea. Hata hivyo mbali na kuwa tatizo la ki-nchi bado tuna nafasi katika yale mazingira tunayoishi. Je, mifumo yetu ya maji nyumbani haikaribiani na mifumo ya maji taka au shimo la taka? Je, tunafagia mazingira yetu nyumbani? Je, tunasafisha kila mara vyoo vyetu? Nyasi ndefu je?. Mazingira yasipokuwa safi ndipo wadudu na vimelea huweza kujipatia hifadhi yao.
JE, WANGAPI VYOO WANAVYOTUMIA HUFANYIWA USAFI MARA KWA MARA?


9.PHYSICAL EXERCISES(mazoezi)
Mazoezi ni muhimu kwa afya. Fanya mazoezi mara kwa mara ni muhimu sana kwa afya yako. Rejea makala:http://www.ntanguligwa.com/2016/07/madhara-ya-kiafya-yanayotarajiwa.html


Yapo mengine mengi ambayo huweza kusababishwa na mfumo wa kisiasa nchini na ya kiserikali na sera zake kama BIMA ZA AFYA, UCHAFUZI WA MAZINGIRA KWA VIWANDA NA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI NA SALAMA, hivi tuwaachie wao tufanye yaliyopo ndani ya uwezo wetu.

MUHIMU: UNAKUJA KUONA KUWA KUKAZANIA KUTIBU UGONJWA HOSPITALINI SIYO TIJA, MAGONJWA YAPO KWENYE JAMII HUKU HUKU TUNAPOISHI NA NDIPO KILA KITU KINAPOANZIA. HIVYO KAMA NI DAWA INAYOFAA INABIDI IWE NI SISI WENYEWE. SISI WENYEWE NDIYO DAWA SAHIHI YA MAGONJWA. TUUNGANE KUTOKOMEZA MAGONJWA KWENYE JAMII ZETU.

HUDUMA DUNI ZA AFYA:

SASA WAJUA:

The food you eat: a fruit a day keeps the doctor away. Information on healthy food must be given to people. These are social determinants of health

Untill next time.

Sunday 14 August 2016

Electronics(part 1)-lesson 5

Welcome and feel at home:In this lesson 5. The topic will be divided into three parts. Ntanguligwa online brings to you Electronics part 1 which thorough covers:1.The band theory of solids 2. Semiconductors 3. Logic gates.

This topic will further be covered by other two lessons as for part 2 and 3 of electronics as per syllabus!



Feel free anytime to contact me 0785071020 normal text and 0714949061 whats app!

Welcome.






Wednesday 10 August 2016

WATANZANIA TUJIFUNZE TABIA YA KUSOMA CONTENTS(YALIYOMO) KWA VITU TUTUMIAVYO- part 1

ENERGY DRINKS
Constantine Ntanguligwa(MD student Muhimbili university of health and allied sciences)
 1230hrs 10th August 2016

Karibu tuzungumze:

Azam kateka sana soko la vinywaji na sekta nyingine za vyakula nchini. Na ni kweli kabisa, vinywaji vyake ni vitamu mno na vya kupendeza.

Lakini kuna hiki kinywaji hapa:

Wengi tumezoea kukiita energy drink kama jina lake linavyojieleza. Ni kweli kabisa kinatuongezea nguvu au pengine ni imani tu tuliyo nayo. Lakini, ni wangapi tumeshawahi kusoma maelekezo yaliyoandikwa kwenye kopo la kinywaji hiki?

Na hivi je?


Moja ya maelekezo ya muhimu yaliyoandikwa kwenye label za vinywaji hivi ni:
  1. Usinywe zaidi ya mbili ndani ya masaa 24 kwa energy drink ya Azam juu.
  2. Usinywe karibu na mda wa kulala.
  3. Red bull yenyewe imeandikwa, wasipewe watoto na wajawazito.
  4. Zimeandikwa pia zina "caffeine".
Pamoja na vinywaji vya aina hiyo vingine vyote.

Shirika la Afya duniani(WHO), liliandika katika makala iliyoandikwa tarehe 14 Oct 2014:
"Increased consumption of energy drinks may pose danger to public health, especially among young people, warns a team of researchers from the World Health Organization Regional Office for Europe in the open-access journal Frontiers in Public Health.

Energy drinks are non-alcoholic beverages that contain caffeine, vitamins, and other ingredients for example, taurine, ginseng, and guarana. They are typically marketed as boosting energy and increasing physical and mental performance.

Researchers reviewed the literature on the health risks, consequences and policies related to energy drink consumption and found reason for concern and basis for further research. The authors conclude that “As energy drink sales are rarely regulated by age, unlike alcohol and tobacco, and there is a proven potential negative effect on children, there is the potential for a significant public health problem in the future”. European Food Safety Authority estimates that 30% of adults, 68% of adolescents, and 18% of children below 10 years consume energy drinks.

The authors suggest several actions to minimize the potential for harm from energy drinks:

  • Establishing an upper limit for the amount of caffeine allowed in a single serving of this type of drinks in line with available scientific evidence;
  • Regulations to enforce restriction of labelling and sales of energy drinks to children and adolescents;
  • Enforcing standards for responsible marketing to young people by the energy drink industry;
  • Training health care practitioners to be aware of the risks and symptoms of energy drinks consumption;
  • Patients with a history of diet problems and substance abuse, both alone and combined with alcohol, should be screened for the heavy consumption of energy drinks;
  • Educating the public about the risks of mixing alcohol with energy drinks  consumption;
  • Further research on the potential adverse effects of energy drinks, particularly on young people.
Energy drinks can be sold in all EU countries, but some countries have introduced regulations, including setting rules for sales to children. Hungary introduced a public health tax that includes energy drinks in 2012. In Sweden, sales of some types of energy drinks are restricted to pharmacies and sales to children are banned."
(retrived 10th Aug 2016 at http://www.euro.who.int/en/health-topics/disease-prevention/nutrition/news/news/2014/10/energy-drinks-cause-concern-for-health-of-young-people)

 Katika mapendekezo yaliyoafikiwa katika kusaidia kupunguza madhara ya vinywaji hivi mengi ni ya kiutawala kwamba viwanda na kampuni vifanye nini. Lakini, sisi tunamchango gani?

Tutachambua mapendekezo yao na kuona nafasi yetu kama watumiaji na wahanga wa vinywaji hivi.

Kwanza, wameelekeza kuandika kwenye vinywaji vyote kuwa haviruhusiwi kwa watoto. Je ni wangapi tunafuata hili? hasa kama hatusomi maelekezo haya, wamemuandikia nani sasa? Wapo watu wengi wanaonunua kinywaji hiki na kuwanywesha watoto wao. Mimi nimekua nikiambiwa na wazazi wangu Red bull ni ya wakubwa(wazazi wajifunze hili pia). Ni mara mia uache kabisa kununua kinywaji hiki uwapo na watoto na kwa wajawazito pia kwani ukinywa wewe ni kama umemnywesha mtoto wako tumboni tayari.

Pili, Kuelimisha watu kuhusu madhara ya kiafya vinywaji hivi vinaweza kusababisha. Kama ninavyokuelimisha sasa, inakupasa uelimishe na wengine pia ili tusaidiane kupunguza madhara kwenye jamii zetu. Pia pale inapobidi kubadilisha mwenendo wa maisha yako(life styles) kuwa tayari kubadilika hasa kwenye kuwapa watoto vinywaji hivi.

MADHARA YA VINYWAJI HIVI NI NINI HASA?

  • Matatizo ya moyo- Premature cardiac contraction. Inaweza kusababisha pia matatizo ya moyo(cardiac arrest-mshtuko wa moyo). Mfano Azam anapokwambia usinywe kabla ya kwenda kulala ni kukusaidia usije kupata mshtuko huo ukiwa usingizini ukakosa msaada ukapoteza maisha.
  • Kukosa usingizi(insomnia) sababu ya kinywaji hiki kukufanya uwe active sana hasa ukinywa zaidi ya kiasi kilichoelekezwa.
  • Baadhi ya dawa unazokunywa haziendani na unywaji wa energy drinks hivyo ni vema kuwa makini unapokuwa kwenye dose na kusababisha vitu kama allergy.
  • Addiction- sababu vinywaji hivi vina caffeine ambapo ukizidisha utakuwa kama mtumiaji wa madawa ya kulevya kwa ku-develop addiction na dependence hasa utakapozidisha kiasi.
  • Kwa watoto huweza kusababisha ukuaji mbovu wa mifupa na kuanza kuwatengenezea matatizo ya moyo taratibu.
  • Inasababisha mishipa ya fahamu(neurones) kuongezeka kusisimka (increase excitability of neurones) huweza kupelekea kutetemeka na kuonekena kama una woga.
Kuna kautamaduni ka kunywa energy drinks kuchanganya na kilevi. Wakiamini kwamba, kwa vile energy drink inaleta nguvu na kukufanya uwe macho(active mda mrefu zaidi) hivyo itakusaidia nguvu ya kunywa pombe nyingi zaidi bila kuchoka na kusikia usingizi.

Hii si kweli hata kidogo, infact ,"In November 2009, the FDA in USA asked manufacturers of alcoholic energy drinks to prove their safety"Seifert S.M et al,(2011). Matokeo yake inasababishia watu wengi kuwa alcohol addicts kwasababu ya imani hiyo.

Seifert S.M et al(2011) pia wanatueleza ,"Energy drinks have no therapeutic benefit, and many ingredients are understudied and not regulated. The known and unknown pharmacology of agents included in such drinks, combined with reports of toxicity, raises concern for potentially serious adverse effects in association with energy drink use (http://pediatrics.aappublications.org/content/127/3/511)
Wanasema kuwa ,vitu ambavyo vipo kwenye energy drinks vimefanyiwa utafiti mdogo sana na haviko regulated kwa kiasi kikubwa hivyo ni vema kuchukua tahadhari.

TUSHIRIKIANE, TUELIMISHANE, TUHAMASISHANE. AFYA YETU PAMOJA.

Until next time.

Monday 8 August 2016

Current electricity (part 2)-lesson 4

Welcome to this lesson 4:

This is last part of the topic. It covers

1. Kirchoff’s laws of electrical networks
2. Conversion of milliammeter to voltmeter and ammeter
3.Current electricity practical details
4. Alternating current
For further questions contact me:0785071020. Don't hesitate to contact me.
Thank you and welcome.





Tuesday 2 August 2016

DRINKING WATER CAN BE DANGEROUS!!!!!

WHEN AM I NOT SUPPOSED TO JUST DRINK WATER?
Constantine Ntanguligwa(MD student Muhimbili university of health and allied sciences)
 2230hrs 2nd August 2016

Karibu tuzungumze:

Inatupasa kunywa maji angalau lita 2 kwa siku. Huu ni msemo ambao katika maisha yetu tumeshawahi kuusikia sehemu. Ni mara ngapi tumeona wenzetu wakitembea na chupa za maji ya kunywa? wengine wenye utaratibu wa kunywa maji mengi asubuhi kabla ya kufanya chochote? Ni ukweli usiopingika kuwa maji ni muhimu sana katika miili yetu.

Damu ni mkusanyiko wa vitu vingi sana. Kwenye damu kuna Cells(white,red and platelets), maji yenyewe(plasma) na zaidi sana madini muhimu kama Sodium, glucose na Potassium.

Damu ndo barabara kuu kwa mifumo mingi mwilini. Mfano, ukitoka kula, baada ya "digestion" chakula husafirishwa kwa damu mwilini kuhifadhiwa sehemu husika. Pia unapo pumua ile oxygen na carbondioxide husafirishwa kwa damu. Pia, uchafu wote wa mwili husafiri kupitia damu kwenda kwenye figo mfano kutengeneza mkojo utoe uchafu huu mwilini. Lakini pia damu husaidia kusambaza joto mwilini na hivyo kubalance joto la mwili.

Kazi zote hizi zitafanyika vizuri pale tu ambapo vitu vyote vinavyotengeneza damu vitakuwa katika uwiano(balance). Chochote kitakachozidi au kupungua kuliko kiasi kinachotakiwa kitaleta madhara makubwa sana mwilini. Hivyo mwili wa binadamu una mfumo maalumu wa kurudisha kwenye uwiano chochote kitakachozidi au kupungua kuliko kawaida mfano usikiaji wa kiu unapopungukiwa maji mwilini ili unywe maji urudishe hali ya kawaida, ni mfumo automatic wa kusaidia kurudisha uwiano.

Mfumo huu utafanya kazi endapo tu uwiano huu hauja athiriwa sana. Kama kuna mabadiliko makubwa sana ya kiasi cha vitu hivi kupungua au kuongezeka sana, mwili unaweza kushindwa kurudisha hali ya kawaida na kupelekea madhara kama kuzimia(kupoteza fahamu).

SABABU ZA UPUNGUFU WA MADINI ZILIZO NDANI YA UWEZO WETU:
Madini ya mwili tunayapata kwenye chakula tunachokula.
  • Mara nyingi, kama mlo wetu usipokuwa na uwiano mzuri tunaweza kujikuta na upungufu wa baadhi ya madini au wingi kupita kiasi. Hivyo tunashauriwa kula vizuri aina zote za vyakula(wanga, vitamin na protini).
  • Pia upungufu huu unaweza kusababishwa na ugonjwa kama minyoo, ugonjwa wa figo, kisukari n.k
  • Pia kutoa damu au kupoteza damu kwenye ajali.
  • Kutokwa jasho(ndo maana jasho linaladha ya chumvi)
  • Haja ndogo(mkojo huwa una madini kutoka mwilini pia ikijaribu kupunguza kiasi kilichozidi)
  • Kutapika na kuharisha


SABABU ZA UPUNGUFU WA MAJI:
Maji mwilini tunayapata kwa kunywa vimiminika, iwe ni maji, juisi au soda. Lakini, maji haya tunayapoteza kwa njia tofauti tofauti sana kama:

  • Kutokwa jasho.
  • Kujisaidia(haja kubwa au ndogo).
  • Kupumua na,
  • Pia kutoa damu au kupoteza damu kwenye ajali. 
  • Kutapika na kuharisha.


Ukichunguza vizuri, kuna namna ambazo zinatufanya tupoteze vyote( madini na maji) mfano kujisaidia haja ndogo tunapoteza maji na madini. Na ndo ntakavyozungumiza hapa hatari inayoweza kutupata tukinywa maji katika hali kama hiyo.
Nitazungumzia kuharisha na kutapika sababu hututokea hasa tukiwa tunaumwa.

HATARI YA KUNYWA MAJI WAKATI WA KUHARISHA AU KUTAPIKA:
Tofauti iliyopo na njia nyingine zinazotufanya tupoteze maji na madini ni kwamba hizi zenyewe husababisha kupoteza kiasi kingi sana cha maji na madini tofauti na njia nyingine. Ndo maana wenye kipindupindu wanapoteza maisha kwa sababu ya kuharisha kupita kiasi na kupoteza maji mengi sana.

Tunapo harisha au kutapika, tukinywa maji tupu yasiyo na kitu chochote(plain water) kitakachotokea ni kwamba utakuwa unaongeza maji peke yake mwilini. Kumbuka umepoteza vyote lakini unarudisha maji tu, hatari iliyopo ni kwamba mwisho wa siku una dilute damu hasa ukinywa maji mengi unaweza ku dilute kufikia kiwango cha hatari na kusababisha ile tunaitwa kwa kitaalamu "hyponatremia" yani sodium iliyopungua kupita kiasi, sababu madini yamepungua sana lakini unaongeza maji na kufanya concentration yake kuwa ndogo zaidi kwenye damu. Hii huweza kupelekea mtu kupoteza fahamu na isipotibiwa haraka huweza sababisha kifo.

TUFANYE NINI WAKATI TUNAHARISHA NA KUTAPIKA?
Tunatakiwa kunywa kitu kitakachorudisha maji na madini kwa pamoja mwilini. Utachukua maji utachanganya sukari na chumvi na kumpa mgonjwa kama huduma ya kwanza ujaribu kuusaidia mwili kurudisha hali ya kawaida. Baada ya hapo mpeleke kwa daktari kwa uchunguzi zaidi.

Maji safi na salama ni uhai. Maji ni muhimu. Kunywa kwa wakati sahihi maji safi na salama!

Mpaka siku nyingine tena. Asanteni


Monday 1 August 2016

Current Electricity(part1)-lesson 3

Welcome to this lesson 3. We are covering extensively about current electricity. The topic will be divided into two parts. This is just part one of the topic. Welcome.

For further questions contact me:0785071020. Don't hesitate to contact me if there are doubts and errors if any in calculations inside the videos.

Corrections: There is a question solved inside where the value of R is indicated as 9.6 ohms, the true answer is 50 ohms. Typing error!

Michael Faraday(1791-1867)-the father and pioneer of electricity.
Feel at home