NANI KAMA MAMA?
Constantine
Ntanguligwa(MD student Muhimbili university of health and allied sciences)
2230hrs 13th July 2016
Kuna msemo maarufu wa nani kama mama? Ni kweli hatukatai
kuwa hakuna kama mama. Je wakina mama/dada, mnajua nguvu mliyonayo katika
kuhakikisha mnaipatia dunia kiumbe kilichochema?
TUTAJIBU MASWALI
MAKUBWA YAFUATAYO MWISHONI:
- UTOAJI MIMBA UNA HASARA GANI KIAFYA?
- SHERIA YA UTOAJI MIMBA INAAGIZA VIPI?
- NI SEHEMU GANI ZA NCHI ZINAONGOZA KWA UTOAJI MIMBA?
- MCHANGO WA MAMA KATIKA UBORA WA MTOTO ATAKAYEZALIWA AKIBEBA UJAUZITO
Karibu tuzungumze,
Utoaji mimba (abortion) ni pale mimba inapotoka bila
kutimiza mda wake sahihi wa mama kujifungua (miezi tisa) kama tulivyozoea
kusema. Hii inaweza kuwa aina mbili:
- · Mimba kutoka yenyewe
- · Mimba kutolewa kwa makusudi
Ni wadada wangapi tumeshawahi kujikuta kwenye kipindi ambapo
tumepata mimba bila kukusudia na kujiuliza niitoe au nisiitoe kwasababu
mbalimbali?
Ni wakaka wangapi tumeshawahi kujikuta kwenye kipindi ambacho
mpenzi wako anapata mimba ambayo hauko tayari kuilea? Na kufanya uamuzi wa
haraka wa kumwambia aitoe nay eye akakataa?
Huku mtaani kwetu mara utasikia jamaa wakimshauri mwenzao, “ah
ukitaka kuitoa, majani ya chai mbona fasta tu?” Mara ngapi wengine wamekuwa
wakitumia spoku na chelewa kujiingiza kwenye njia za uzazi kujaribu kuitoa
mimba? Je ni kweli tunajua tunachokifanya?
Katika Muhimbili University of health and allied sciences
scientific conference mwaka HUU 2016 mtalaamu mmoja Prof. Muganyizi (mtalamu wa afya
ya kina mama) alieleza kwa kina kuhusu hili. Alisema:
·
Kwa nchi yetu Tanzania, UTOAJI MIMBA UNARUHUSIWA
PALE TU AMBAPO AFYA YA MAMA IKO HATARINI. Swali ni je, nani wa kuitoa mimba
hiyo?
·
Tanzania katika mimba kumi, nne hazikutarajiwa.
·
Kati ya hizo zisizotarajiwa 15% hutolewa kwa
makusudi na 5% huishia kutoka zenyewe.
IMAGINE IF IT WAS YOUR OWN MOM WHO DID THIS TO YOU, WHERE COULD YOU BE?!!!! |
Kinachotisha hapo ni
kwamba wengi 40% waliotoa mimba wanaishia kupata matatizo makubwa sana ya
kiafya kama:
- Kupoteza maisha kwa kupoteza damu nyingi mtoto anapotoka
- Kupasuka kwa mfuko wa uzazi hivyo kushindwa kuzaa tena
- Kuharibu njia za uzazi (cervix)
- Matatizo ya kisaikolojia n.k
,” Under the Penal
Code, section 230, termination of
pregnancy is lawful where it is done to preserve the life or health of the
pregnant woman. 150 – Any Person
who, with intent to procure miscarriage of a woman, whether she is or is not
with child, unlawfully administers to her or causes her to take any poison or
other noxious thing, or uses any force of any kind, or uses any other means
whatever, is guilty of a felony, and is liable to imprisonment for fourteen
years. 151- Every woman being with child who with intent to procure her own
miscarriage unlawfully administers to herself any poison or other noxious
thing, or uses any force of any kind, or uses any other means whatsoever, or
permits any such thing or means to be administered or used to her, is guilty of
a felony, and is liable to imprisonment for seven years. 152- Any person who unlawfully supplies to or
procures for any person anything whatsoever, knowing that it is intended to be
unlawfully used to procure the miscarriage of a woman, whether she is or is not
with child, is guilty of a felony, and is liable to imprisonment for three
years. Section 219 (1) - Subject as
hereinafter in the subsection provided, any person who with intent to destroy
the life of a child capable of being born alive, by an wilful act causes a
child to die before it has an existence independent of its mother, shall be
guilty of the felony of ‘child destruction’, and shall be liable on conviction
to imprisonment for life; Provided that no person shall be guilty of an offence
under this section unless it is proved that the act which caused the death of
the child was not done in good faith for the purpose only of preserving the
life of the mother.”
Ni kweli kila mtu anatamani kuwa na mtoto mwenye akili za darasani. Mtoto msikivu. Mtoto mzuri ambapo akitajwa utasema kwa haraka sana “kuwa huyo ni mwanangu jamani.” Wengi na tunaamini kuwa vitu hivi hutokea tu kwa kufuata historia za ukoo. Ni kweli hatukatai lakini kama mama na baba kuna mchango mkubwa sana unaoweza kutoa/kutengeneza mazingira ya kupata watoto wa aina hii tunaowataka.
Kwa ufupi. Safari nzima ya uzazi tunaigawa sehemu tatu (trimester).
·
I- wiki ya 1 mpaka ya 13
·
II- wiki ya 14 mpaka ya 26
·
III- wiki ya 27 mpaka ya 39
Safari nzima ya wiki kama 39 hivi (miezi tisa)
- Stage I acha kabisa vilevi, sigara , vipodozi , Mionzi mikali (kama X rays) na Vichafuzi mazingira vyenye nguvu
- Stage III kuwa makini na nguo unazovaa, kwa ujumla ulinde tumbo lako lisipate usumbufu wowote kwasababu stage hii physical injuries ni hatari zaidi.
- Jilinde, kula vizuri kwasababu kila unachokula na kunywa mtoto naye anakula na kunywa hicho hicho.
- Tembelea wodini walau mara moja kila mwezi.
Zingatieni haya na mtoto wenu atakua mwenye afya nzuri na
aliyelelewa vizuri tangu tumboni mwa mama.
Vifo vya kina mama na watoto wenye umri chini ya miaka
mitano ni vingi mno. KAMWE USIKUBALI KUJIFUNGULIA NYUMBANI. OKOA MAISHA YA
MTOTO. HAKIKISHA SAFARI YAKE YA KUJA DUNIANI INAKUA NJEMA NA SALAMA.
KULINDA AFYA YA MAMA NA MTOTO NI MIMI NA WEWE.
Somo Zuri mno..blecd alweiz Mr.doctor
ReplyDeleteasante... wafundishe na wengine
DeleteGud bro ngamesha hapa
ReplyDeleteGud bro ngamesha hapa
ReplyDeleteSomo kwel n zur kbx
ReplyDeleteSomo zuri sana,asante sana
ReplyDelete