Monday, 18 July 2016

BE INFORMED, ITS YOUR RIGHT AND ITS FREE. AFYA KWANZA NDO KAULI MBIU

TOO COMMON TO BE COMMON
Constantine Ntanguligwa(MD student Muhimbili university of health and allied sciences)
10.04 AM, 6th July 2016

Karibu tuzungumze,

Leo tutajifunza vitu vinne ambavyo tunavijua na kuviskia na pengine kupitia hali hizi baadhi ya mda. Navyo ni:
  1.          HIKI KITU TUNAITA “JINAMIZI” LINALOTUKABA TUKIWA TUMELALA USIKU NI NINI?
  2.            ASUBUHI NIKIAMKA, MBONA NIKIKANYAGA CHINI KISIGINO KINAUMA?
  3.          HIVI, TUNAPOSIKIA MCHEZAJI KAPATA “HAMSTRING” INJURY, NJE MIEZI SITA. HIVI HIZI HARMSTRING NI NINI?


Ni haki yako kufahamu mambo yanayohusu afya yako kwa ujumla, basi twende kazi!

JINAMIZI
Ni mara nyingi tuna ndugu zetu au sisi wenyewe tumeshawahi kusikia kama tunakabwa usiku na kwa mazoea asubuhi yake huwa tunawambia watu ,”aisee, jana usiku nilikabwa na Jinamizi”.
Mtu wangu wa nguvu, Mungu wetu ni wa ajabu sana kwani huwezi amini hii ni hali ya kiafya iliyowekwa ili ikusaidie.
Mara nyingi hii ni dalili ya matatizo ya moyo. Tatizo husika hapa linaitwa “cardiac failure”. Tatizo hili huja pale ambapo Moyo wako unashindwa kusukuma damu ya kutosha ili kufika sehemu zote za mwili zinazohitaji damu.
Usiku unapokuwa umelala, kwasababu ni tofauti na ukiwa umesimama ambapo angalau force of gravity inasaidia kuvuta damu chini, sehemu kama za kwenye miguu hivyo kuisaidia damu kusambaa.
Hivyo unapolala damu inaishia kujikusanya maeneo ya juu ya mwili hasa kifuani kuchangiwa na tatizo hilo la moyo kushindwa kusukuma damu vizuri na kusababisha mtu kusikia kama kitu kizito kina kukaba au kukubana sana maeneo ya kifuani kuja juu.
Ndio maana watu wa namna hii watashtuka usiku ili damu isambae sehemu nyingine za mwili pale anaposhtuka na kuinuka.
Hivyo ni vema ukamwona daktari mapema ili kukufanyia uchunguzi Zaidi.

KISIGINO KUUMA ASUBUHI
Mwili wa binadamu ni kitu kilichotengenezwa kwa umakini sana kisigino chako kimeumbwa kubeba uzito wako siku nzima unapotembea.
 Kisigino chako ni moja ya mfupa iliopo miguuni. Mfupa huu kwa chini(kwenye nyayo) kuna tishu inayoitwa kitalamu “Plantar fascia” inayoiunganisha na sehemu ya mbele ya mguu wako.
Tishu hii maskini inakumbana na mengi kila siku kutegema na utembeaji wa mtu na kwa kawaida inasaidia sana kulinda nyayo hasa sehemu yake ya katikati.
Kwa watu ambao wanatembea sana au kusimama kwa mda mrefu sana au chochote kitakachopeleka pressure kubwa kwenye kisigino hivyo kuilazimu kufanya kazi kuliko kawaida (overstretching) , kuna uwezekano wa kuumiza tishu hii hivyo kuisababisha kuvimba.
Itakapovimba ndipo kisigino kitakapokuwa kigumu na kuwa na maumivu kama uvimbe mwingine tu na kuja kushtuka asubuhi unapoamka na kuanza kutembea.
Unaweza kupunguza maumivu kwa kufanya zoezi la kunyosha nyosha mguu wako ukistretch unyayo wako na kupumzisha miguu yako. Uvimbe huu utapungua na kuisha.

HARMSTRING
Mara nyingi kwenye mpira wa miguu tumeona wachezaji wanapigiwa pasi wanaiacha ipite tu na kushindwa kuifanyia chochote hata baada ya hapo huishia kushika nyuma ya paja chini kidogo na kuomba kutolewa. Baada ya hapo tunasikia, “nje miezi sita”
Harmstring ni mkusanyiko wa misuli mitatu(majina yake ni magumu kidogo kitaalamu). Misuli hii ipo sehemu ya nyuma ya paja sehemu yote mpaka kushuka chini karibu na usawa wa goti.
Kazi kubwa ya misuli hii ni kukunja goti. Hivyo ukizi “over stretch” hizi muscles ndipo tatizo huanza la “harmstring” injury hivyo kushindwa kukunja goti au kukunja goti kwa maumivu makali. Hii hutibiwa kitaalamu na watalamu wa mambo ya mifupa na misuli (orthopaeditricians)

That’s all for today.


No comments:

Post a Comment