Thursday, 18 August 2016

VICIOUS CIRCLE OF SOCIAL DETERMINANTS OF HEALTH

HEALTH AND THE CURATIVE APPROACH
Constantine Ntanguligwa(MD student Muhimbili university of health and allied sciences)
 0945hrs 18th August 2016

Karibu tuzungumze:

Kwanza nianze kwa kuelezea maana ya "vicious circle". Huu ni mzunguko wa mfumo kama wa duara unahusisha kitu flani na sababu zake kuwa na mwendelezo usioisha. Tunaposema "vicious circle of social determinants of health" tunamaanisha duara linaloanza na Afya yako na yale yote yanayoweza kufanya afya yako kuwa bora au kuidhoofisha katika uhusiano usio na kikomo. Ni dhahiri kwamba, duara huzunguka bila mwisho

Pili, tunaposema "curative approach" huu ni mfumo wa ki-tiba ambao hukazia zaidi kwenye matibabu ya mgonjwa mwenyewe moja kwa moja, mfumo ukizingatia hasa vijidudu vinavyokufanya uumwe na vyanzo. The center of focus kwenye mfumo huu wa tiba vina concentrate zaidi kwa vimelea kama chanzo kikuu cha magonjwa (parasites and vectors as primary to health). Huu ndo mfumo tunaotumia katika sekta yetu ya afya hapa.



Watalamu wa sayansi ya tabia(behavioural sciences) wanatuambia, vitu vilivyo msingi kwa afya ambavyo ndivyo vitakavyoamua afya yako kesho itakuwaje(social determinants of health), si mbu wala nzi wala vimelea vya homa, lakini ni hivi vifuatavyo:

1.LIFE STYLES(mienendo ya maisha yetu)
Hizi ni tabia/mienendo yetu ya kila siku. Je, tunakunywa pombe sana? Je, tuna wapenzi wengi? Je tunafanya ngono zembe? Je,tunakula kabla ya kunawa? Hii yote ndiyo itakayoamua afya yako wewe itakuwaje, kama ni magonjwa ya zinaa yatakuwa rafiki yako au homa ya tumbo na kipindupindu. Sigara inauwa watu milioni 6 kila mwaka inazidi idadi ya watu wanaokufa kwa UKIMWI, TB na MALARIA ukijumuisha kwa mwaka.
JE, MIENENDO YETU YA MAISHA NI RAFIKI KWA AFYA ZETU?



2.AGE(umri)
Umri unachangia sana baadhi ya magonjwa. Mfano, si ajabu kuanzia umri wa miaka 30 na kuendelea kupata magonjwa ya moyo, figo, kisukari na presha, labda kwasababu ya misuli na mishipa ya damu kuanza kuchoka. Si, ajabu watoto wadogo kupata minyoo labda kwasababu ya kula kila wanachoweka mikononi bila kujua hali ya usafi na usalama. Si ajabu vijana wengi kuwa wahanga wa magonjwa ya zinaa na madawa ya kulevya labda kutokana na ushawishi wa makundi na tamaa. Si ajabu vijana wengi kuwa wahanga wa ajali za boda boda labda kwasababu wao ndo watafutaji maisha wakubwa katika umri huo.
JE, TUNATAMBUA UMRI WETU HUWEZA KUPATWA NA MAGONJWA GANI ZAIDI NA YALE YA WATOTO WADOGO WANAOHITAJI USIMAMIZI WETU?


3.CULTURE(tamaduni)
Hapa ndipo zinapokuja mila na desturi. Hivi ni kweli unakubali kurithishwa mke wa kaka yako bila kujali uhusiano wao ulikuwaje? kama ana ukimwi je? Ni kweli mila na desturi zetu zinatuambia tukae na wanyama wetu ndani ya nyumba zetu? Usalama wa magonjwa ya wanyama kutokua yetu uko wapi?
Ni kweli watoto wetu wa kike wanakeketwa mpaka leo hii? Afya yao ya uzazi, saikolojia na magonjwa ambukizi i hali gani? Hivi ni kweli kuna makabila ambayo kumpiga mke wako ni lazima, kufanya uzazi wa mpango ni mwiko na kujifungulia nyumbani ndo mpango mzima? Nani kama mama inakujaje sasa hapo? Pamoja na mila na desturi nyingine nyingi sana.
JE, UKO TAYARI KUBADILI MILA NA DESTURI ZINAZOHATARISHA AFYA YAKO NA MAISHA SASA?


4.GENDER(jinsia)
Ni kweli kabisa, ukiwa mwanaume kuna magonjwa yanayokuhusu na ukiwa mwanamke kuna ya kwako pia. Hivyo, kuwa na jinsia tayari na chanzo cha magojwa fulani mfano kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi kwa wanawake lakini pia tatizo la nguvu za kiume kwa wanaume. Labda ndo maana tunawatalamu kama wanaoitwa madaktari wa kina mama(gynaecologists). Takwimu zinaonesha pia kuwa, wanawake hutembelea hospitali mara nyingi zaidi kuliko wanaume. Labda kwasababu wanamatatizo mengi zaidi au kwasababu wanaume hujikuta wako imara na kwenda hospitali utaonekana dhaifu. Labda nikwambie tu kuwa, kirusi cha ukimwi kikikuingia, hakijali wewe ni mwanaume au mwanamke.
JE, TUNATAMBUA MAGONJWA YANAYOIKUMBA JINSIA YETU(ANGALAU MACHACHE MUHIMU) ILI KUJILINDA?

5.EDUCATION(elimu)
Ni kweli, mtu ambaye ameenda shule walau elimu ya msingi ni tofauti sana na yule ambaye hajaenda kabisa. Angalau nikiwaangalia wadogo zangu mmoja yupo chekechea na mwingine darasa la nne, kabla ya kula wana nawa mikono. Wanajua maji wanayotakiwa kunywa inabidi yachemshwe kwanza. Wewe mwenye elimu kubwa zaidi tunategemea uwe na uelewa mkubwa zaidi na uwezo wa kuepuka vyanzo vya magonjwa vinavyoepukika. Maajabu yanakuja pale ambapo leo hii mwanafunzi wa form 6 anapokunywa maji ya bomba bila kuchemsha au mwanafunzi wa chuo kikuu anapokula bila kunawa. Hadi hili tutailaumu serikali kuwa kuna mfumo mbovu wa elimu? Ni uzembe na kutozingatia yale tunayoyajua. Namna hii magonjwa yataendelea kuwa rafiki zetu. Leo hii nchi kama Denmark ukiona mbu basi ni utalii umefanya. Malaria ni historia. Kwanini uwe ghala la vimelea na elimu yote uliyonayo? Basi fanya vile vinavyowezekana kutokana na elimu uliyopata uepuke baadhi ya magonjwa. Elimu si ya darasani tu, familia ndiyo shule ya kwanza kwenye maisha ya binadamu. Kuwa msimamizi wa afya nyumbani na mahali unapoishi.

JE, ELIMU ULIYONAYO INAKUSAIDIA KUWA NA AFYA YA TOFAUTI NA ASIYEKUWA NAYO?


6.WORKING CONDITIONS(mazingira ya kazi)
Ni kweli wanasema, mfanikiwa hachagui wala kubagua kazi. Ni kweli hali za maisha yetu zinaweza kutupelekea kufanya kazi zinazoweka afya zetu matatani, na mara nyingine ipo nje ya uwezo wetu. Mtu unapolazimika kufanya kazi kama msafisha jiji, mda wote uko na uchafu wa jalalani, unafanya kazi kiwanda cha cement au mashine ya kukoboa mda wote uko na vumbi kali au kwenye minara ya simu mda wote upo kwenye mionzi hatarishi kwa kansa. Muhimu ni kuzingatia utendaji wa kazi tujilinde inavyowezekana. Kama ni jalalani, tuvae gloves, kama ni mionzi tujitahidi kupunguza kukaa maeneo hayo bila sababu, kama ni vumbi kali tukumbuke kuvaa mask usoni. Mwingine atasema, kama ni kahaba au changudoa uvae kondomu ujilinde. Inaweza kuwa sawa unajilinda lakini hiyo ni tofauti. Kama ni kazi fanya kazi halali zenye risk kidogo sababu hatari ipo katika kazi zote zinatofautiana tu uzito. Hata daktari yupo kwenye hatari kubwa ya maambukizi kutoka kwa wagonjwa.
JE, UNAFAHAMU MAZINGIRA YA KAZI YAKO YANA HATARI GANI KWA AFYA YAKO?
 


7.NUTRITION(vyakula):
Mwili wetu hufanya kazi vizuri pale tu ambapo tutakuwa tumeshiba vizuri. Ni wangapi wanaweza kukaa kwa makusudi siku nzima masaa 24 bila kula chochote wakaishi bila shida yoyote, comfortably. Mara zote tutahitaji kula, je tunakula nini? Mlo wetu unafaa kuitwa chakula bora. Tunatakiwa kula matunda kwa sana, kunywa maji kwa sana na kuhakikisha mlo wetu una mahitaji yote katika kiasi sahihi. Wanga kidogo(vyakula kama mihogo,ugali,wali na viazi), protini kigodo(samaki,nyama,mayai), mafuta kidogo(karanga,vyakula vya kukaanga kama chipsi), vitamini(mboga za majani na matunda). Tujitahidi tuwe tunapata hivi angalau kila siku na kupunguza ulaji wa vyakula vya mafuta na kuongeza matunda(somo hili refu kidogo tutalitafutia makala yake).

JE, WANGAPI SISI MLO NI CHIPSI,KUKU,PIZZA NA BURGER TU MASAA 24 SIKU SABA KATIKA WIKI. TUNAJIANDAA KUWA DILI KWA MADAKTARI WA MOYO?

8.ENVIRONMENT(mazingira)
Uchafuzi wa mazingira ni tatizo kubwa sana katika nchi zetu zinazoendelea. Hata hivyo mbali na kuwa tatizo la ki-nchi bado tuna nafasi katika yale mazingira tunayoishi. Je, mifumo yetu ya maji nyumbani haikaribiani na mifumo ya maji taka au shimo la taka? Je, tunafagia mazingira yetu nyumbani? Je, tunasafisha kila mara vyoo vyetu? Nyasi ndefu je?. Mazingira yasipokuwa safi ndipo wadudu na vimelea huweza kujipatia hifadhi yao.
JE, WANGAPI VYOO WANAVYOTUMIA HUFANYIWA USAFI MARA KWA MARA?


9.PHYSICAL EXERCISES(mazoezi)
Mazoezi ni muhimu kwa afya. Fanya mazoezi mara kwa mara ni muhimu sana kwa afya yako. Rejea makala:http://www.ntanguligwa.com/2016/07/madhara-ya-kiafya-yanayotarajiwa.html


Yapo mengine mengi ambayo huweza kusababishwa na mfumo wa kisiasa nchini na ya kiserikali na sera zake kama BIMA ZA AFYA, UCHAFUZI WA MAZINGIRA KWA VIWANDA NA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI NA SALAMA, hivi tuwaachie wao tufanye yaliyopo ndani ya uwezo wetu.

MUHIMU: UNAKUJA KUONA KUWA KUKAZANIA KUTIBU UGONJWA HOSPITALINI SIYO TIJA, MAGONJWA YAPO KWENYE JAMII HUKU HUKU TUNAPOISHI NA NDIPO KILA KITU KINAPOANZIA. HIVYO KAMA NI DAWA INAYOFAA INABIDI IWE NI SISI WENYEWE. SISI WENYEWE NDIYO DAWA SAHIHI YA MAGONJWA. TUUNGANE KUTOKOMEZA MAGONJWA KWENYE JAMII ZETU.

HUDUMA DUNI ZA AFYA:

SASA WAJUA:

The food you eat: a fruit a day keeps the doctor away. Information on healthy food must be given to people. These are social determinants of health

Untill next time.

5 comments:

  1. Its very nice as it has reminded me what I'm supposed to do especially to the community towards attaining sustainable health.thanx in advance.

    ReplyDelete
  2. Its very nice as it has reminded me what I'm supposed to do especially to the community towards attaining sustainable health.thanx in advance.

    ReplyDelete
  3. Leo nimejifunza kitu kizuri sana. Kilichobaki ni utekelezaji. Somo zuri, pia linaeleweka. Good job.

    ReplyDelete