WHEN AM I NOT SUPPOSED TO JUST DRINK WATER?
Constantine Ntanguligwa(MD student Muhimbili university of health and allied sciences)2230hrs 2nd August 2016
Karibu tuzungumze:
Inatupasa kunywa maji angalau lita 2 kwa siku. Huu ni msemo ambao katika maisha yetu tumeshawahi kuusikia sehemu. Ni mara ngapi tumeona wenzetu wakitembea na chupa za maji ya kunywa? wengine wenye utaratibu wa kunywa maji mengi asubuhi kabla ya kufanya chochote? Ni ukweli usiopingika kuwa maji ni muhimu sana katika miili yetu.
Damu ni mkusanyiko wa vitu vingi sana. Kwenye damu kuna Cells(white,red and platelets), maji yenyewe(plasma) na zaidi sana madini muhimu kama Sodium, glucose na Potassium.
Damu ndo barabara kuu kwa mifumo mingi mwilini. Mfano, ukitoka kula, baada ya "digestion" chakula husafirishwa kwa damu mwilini kuhifadhiwa sehemu husika. Pia unapo pumua ile oxygen na carbondioxide husafirishwa kwa damu. Pia, uchafu wote wa mwili husafiri kupitia damu kwenda kwenye figo mfano kutengeneza mkojo utoe uchafu huu mwilini. Lakini pia damu husaidia kusambaza joto mwilini na hivyo kubalance joto la mwili.
Kazi zote hizi zitafanyika vizuri pale tu ambapo vitu vyote vinavyotengeneza damu vitakuwa katika uwiano(balance). Chochote kitakachozidi au kupungua kuliko kiasi kinachotakiwa kitaleta madhara makubwa sana mwilini. Hivyo mwili wa binadamu una mfumo maalumu wa kurudisha kwenye uwiano chochote kitakachozidi au kupungua kuliko kawaida mfano usikiaji wa kiu unapopungukiwa maji mwilini ili unywe maji urudishe hali ya kawaida, ni mfumo automatic wa kusaidia kurudisha uwiano.
Mfumo huu utafanya kazi endapo tu uwiano huu hauja athiriwa sana. Kama kuna mabadiliko makubwa sana ya kiasi cha vitu hivi kupungua au kuongezeka sana, mwili unaweza kushindwa kurudisha hali ya kawaida na kupelekea madhara kama kuzimia(kupoteza fahamu).
SABABU ZA UPUNGUFU WA MADINI ZILIZO NDANI YA UWEZO WETU:
Madini ya mwili tunayapata kwenye chakula tunachokula.
- Mara nyingi, kama mlo wetu usipokuwa na uwiano mzuri tunaweza kujikuta na upungufu wa baadhi ya madini au wingi kupita kiasi. Hivyo tunashauriwa kula vizuri aina zote za vyakula(wanga, vitamin na protini).
- Pia upungufu huu unaweza kusababishwa na ugonjwa kama minyoo, ugonjwa wa figo, kisukari n.k
- Pia kutoa damu au kupoteza damu kwenye ajali.
- Kutokwa jasho(ndo maana jasho linaladha ya chumvi)
- Haja ndogo(mkojo huwa una madini kutoka mwilini pia ikijaribu kupunguza kiasi kilichozidi)
- Kutapika na kuharisha
SABABU ZA UPUNGUFU WA MAJI:
Maji mwilini tunayapata kwa kunywa vimiminika, iwe ni maji, juisi au soda. Lakini, maji haya tunayapoteza kwa njia tofauti tofauti sana kama:
- Kutokwa jasho.
- Kujisaidia(haja kubwa au ndogo).
- Kupumua na,
- Pia kutoa damu au kupoteza damu kwenye ajali.
- Kutapika na kuharisha.
Ukichunguza vizuri, kuna namna ambazo zinatufanya tupoteze vyote( madini na maji) mfano kujisaidia haja ndogo tunapoteza maji na madini. Na ndo ntakavyozungumiza hapa hatari inayoweza kutupata tukinywa maji katika hali kama hiyo.
Nitazungumzia kuharisha na kutapika sababu hututokea hasa tukiwa tunaumwa.
HATARI YA KUNYWA MAJI WAKATI WA KUHARISHA AU KUTAPIKA:
Tofauti iliyopo na njia nyingine zinazotufanya tupoteze maji na madini ni kwamba hizi zenyewe husababisha kupoteza kiasi kingi sana cha maji na madini tofauti na njia nyingine. Ndo maana wenye kipindupindu wanapoteza maisha kwa sababu ya kuharisha kupita kiasi na kupoteza maji mengi sana.
Tunapo harisha au kutapika, tukinywa maji tupu yasiyo na kitu chochote(plain water) kitakachotokea ni kwamba utakuwa unaongeza maji peke yake mwilini. Kumbuka umepoteza vyote lakini unarudisha maji tu, hatari iliyopo ni kwamba mwisho wa siku una dilute damu hasa ukinywa maji mengi unaweza ku dilute kufikia kiwango cha hatari na kusababisha ile tunaitwa kwa kitaalamu "hyponatremia" yani sodium iliyopungua kupita kiasi, sababu madini yamepungua sana lakini unaongeza maji na kufanya concentration yake kuwa ndogo zaidi kwenye damu. Hii huweza kupelekea mtu kupoteza fahamu na isipotibiwa haraka huweza sababisha kifo.
TUFANYE NINI WAKATI TUNAHARISHA NA KUTAPIKA?
Tunatakiwa kunywa kitu kitakachorudisha maji na madini kwa pamoja mwilini. Utachukua maji utachanganya sukari na chumvi na kumpa mgonjwa kama huduma ya kwanza ujaribu kuusaidia mwili kurudisha hali ya kawaida. Baada ya hapo mpeleke kwa daktari kwa uchunguzi zaidi.
Maji safi na salama ni uhai. Maji ni muhimu. Kunywa kwa wakati sahihi maji safi na salama!
Mpaka siku nyingine tena. Asanteni
No comments:
Post a Comment