HEDHI
SALAMA ZISIZO NA MAUMIVU
Helleminigilder Ndangalasi (MD student Muhimbili university of health and allied sciences)
0030hrs
16th July 2016
Labda sio mara nyingi lakini nimekutana na wanawake
mbalimbali wakilalamika kuhusu kupata hedhi zinazoambatana na maumivu kile
watalamu wanaita “dysmenorrhea”. Mimi mwenyewe nikiwa mhanga wa hili mara
nyingi mpaka pale nilipopata suluhisho. Ndipo nilipojua, anha… Kumbe na mimi
naweza kupata hedhi zisizokuwa na maumivu yoyote.
BASI
LEO TUTAJIBU MASWALI MAKUU MAWILI:
1.NINI
KINASABABISHA MAUMIVU HAYA?
2.
NTAFANYAJE KUPATA SULUHISHO LA HII HALI?
Karibu
tuzungumze,
Hedhi kwa kawaida , ile damu hutoka
kwasababu yai ulilotengeneza ili lirutubishwe na shahawa za mwanaume kwa bahati
mbaya halijarutubishwa hivyo hilo yai pamoja na kuta za mfuko wa uzazi
zilizoandaliwa kumpokea mtoto ambaye angeanza kutengenezwa vinatolewa sababu
havina kazi tena kwa mda huo. Labda kwasababu haukujamiiana na mwanaume yai
lilipotengenezwa au labda mlitumia kinga hivyo shahawa hazikufika kwenye yai.
Maumivu
kwenye hedhi husababishwa na kemikali mwilini kitalamu zinaitwa
“prostaglandins”. Hizi kazi yake kubwa ni kufanya misuli ya mfuko wa uzazi
(uterus) kukakamaa kana kwamba kuna mtoto mwanamke ajifungue. Ndizo hata
zinaleta uchungu wa mama anayetaka kujifungua. Sasa kwa baadhi ya wanawake
wakati wa hedhi, kemikali hizi hutengenezwa hivyo kufanya misuli hii ya mfuko
wa uzazi kukamaa kuliko kawaida mpaka kupelekea maumivu.
TUFANYEJE
KAMA WANAWAKE?
Kabla sijasema hili kwanza naomba
tukumbushie tu haraka haraka jinsi ya kuhesabu mzunguko wa hedhi ambao kwa
kawaida ni wa siku kama 28 hivi.
Je, unakumbuka mara ya mwisho ulivyopata
hedhi? Hi indo ilikua siku ya kwanza ya mzunguko huo. Hedhi huwa zinaweza
kuchukua siku 3 mpaka 5 kwa wengine. Siku ya 14 kuanzia siku ya kwanza ya hedhi
au siku moja kabla au baada ndipo yai linatolewa tayari kurutubishwa. Kama
likirutubishwa, utapata ujauzito lakini kama lisipo rutubishwa tunategema
litatoka kama hedhi baada ya siku kama 14 nyingine utakapoanza mzunguko mpya.
Jumla huwa siku kwa kawaida 28 ingawa zinaweza kuongezeka au kupungua kutokana
na vitu kama msongo wa mawazo(stress) lakini ni vizuri ukamwona daktari kwa
uchunguzi zaidi.
Ukiwa unapata hedhi zenye maumivu KAMWE USIKIMBILIE KUNYWA DAWA ZA KUTULIZA
MAUMIVU KAMA PANADOL HASA BILA USHAURI WA DAKTARI, TUMIA PALE UNAPOSHAURIWA NA
DAKTARI TU.
Jiwekee
utaratibu wa kufanya mazoezi ya mwili siku zinazokaribia
siku ya 14, kuanzia siku ya 12 mpaka 16 hivi. Ruka Kamba , kimbia ukiweza
n.k. Vizuri kama ukifanya mazoezi kuwa sehemu yako ya maisha kabisa ukiachana
na siku za hedhi tu, ina umuhimu mkubwa wa kiafya pia ukizingatia itakutengezea
mwili unaovutia.
TUFANYE MAZOEZI. MIMI NACHEZA BASKETBALL, WEWE JE? #MSOLWA SEC SCHOOL |
Vaziri et al.,(2015) anatuambia, ”Both aerobic and stretching exercises were effective
in reducing the severity of dysmenorrhea. Therefore, women could choose one of
these two methods with regard to their interest and lifestyle.”
Mtalamu
mwingine aliyafanya tafiti yake kwa kuangalia mazoezi ya Yoga yanapunguzaje
hedhi zenye maumivu akahitimisha kuwa,” yoga interventions may reduce menstrual
cramps and menstrual distress in female undergraduate students with primary
dysmenorrhea”.(Yang & Kim, 2016)
Pia Ortiz et al (2015) anasema ,”Strengthening, stretching and muscle relaxation
techniques, in addition to jogging, are effective for reducing dysmenorrheic
symptoms when they are regularly performed.”
TAHADHARI:
MAUMIVU YAKIZIDI AU YAKIENDELEA MUONE DAKTARI HARAKA, KUNA UWEZEKANO WA
MAGONJWA MENGINE KUWA CHANZO KAMA “ENDOMETRIOSIS” (TUTAZUNGUMZIA SIKU NYINGINE)
Tafadhali wasiliana nasi, tujulishe kama
imekusaidia na pia kama una maswali.
Mpaka tutakapokutana siku nyingine.
Asanteni sana
References:
Ortiz MI1, Cortés-Márquez SK2, Romero-Quezada LC3,
Murguía-Cánovas G4, J.-D. A. (2015). Effect of a physiotherapy program in women
with primary dysmenorrhea. Retrieved from
http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/26319652
Vaziri, F., Hoseini, A., Kamali, F., Abdali, K., Hadianfard,
M., & Sayadi, M. (2015). Comparing the effects of aerobic and stretching
exercises on the intensity of primary dysmenorrhea in the students of
universities of bushehr. Journal of Family & Reproductive Health, 9(1),
23–8. Retrieved from http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/25904964
Yang, N.-Y., & Kim, S.-D. (2016). Effects of a Yoga
Program on Menstrual Cramps and Menstrual Distress in Undergraduate Students
with Primary Dysmenorrhea: A Single-Blind, Randomized Controlled Trial. Journal
of Alternative and Complementary Medicine (New York, N.Y.).
http://doi.org/10.1089/acm.2016.0058
No comments:
Post a Comment